Thursday, 24 November 2016

AJARI MBAYA YATOKEA IFAKARA

Prado na T 539 DHL ikielekea Ifakara Leo SAA 7 mchana imegonga Train ya Udzungwa iliyokuwa inaelekea Kidatu/Kilombero na kupitia tukio hilo Watu wawili waliokuwa kwenye Prado wamefariki papo hapo.Yeyote anayeijua gari hiyo namjuza afike Ifakara St Francis Hosp kwa hatua zaidi.

Thursday, 17 November 2016

Urefu wamtesa Baraka Elias wa Tanzania

Baraka Elias Mashauri, ni kijana Mtanzania mrefu wa futi 7.4, urefu wake usio wa kawaida umemfanya kushindwa kupata matibabu ya kubadilishiwa nyonga baada ya kuanguka nyumbani kwake.
Akizungumza na mwandishi wetu akiwa nyumbani kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Elias amesema ameshindwa kupata matibabu kwa sababu kimo chake.
Elias alipelekwa kwenye Taasisi ya tiba ya mifupa ya Muhimbili, MOI kwa ajili ya uchunguzi wa madaktari, akitokea mkoa wa Ruvuma kusini mwa Tanzania, baada ya kukosa huduma kwa kile kilichoelezwa kutokuwa na wataalam na vifaa vya kumtibu
''Madaktari wa MOI wamesema kuwa vifaa walivyonavyo na wagonjwa waliozoea kuwahudumia ni tofauti na mimi," amesema.
"Hata vifaa vya X-Ray haviwezi kutoa picha halisi ya kuona ukubwa wa kifaa wanachopaswa kuniwekea, pia wamesema vitanda vya kulaza wagonjwa wakifanyiwa upasuaji ni vifupi kwa kuwa mgonjwa anapaswa mwili wote uenee kitandani''.

Kutokana na hali hiyo Elias sasa anasubiri majibu ya madaktari ambao wanafanya mazungumzo na wenzao wanaoshirikiana nao katika shughuli za kitabibu nje ya Tanzania, ili aweze kupata matibabu.

Kurithi

Elias amesema jamii inayomzunguka hushangaa urefu wake, lakini anasema kwake anaona kawaida tu kwa kuwa wazazi wake walimweleza kuwa urefu wake ni wa kurithi.
''Upande wa familia ya Baba na Mama babu zao wote walikuwa warefu kwa hiyo hii hali nafikiri imesababishwa na vinasaba''.

Raisi wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri ametia saini Sheri za huduma za habari

Rais wa wa Tanzania John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ambayo imekuwa ikipingwa na wadau katika sekta ya uanahabari nchini humo.
Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge la Tanzania Jumamosi 5 Novemba mjini Dodoma.
Taarifa kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya rais imesema Rais Magufuli alitia saini Sheria hiyo tarehe 16 Novemba na kwamba anaamini sheria hiyo itakuwa na manufaa mengi.
"Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa," amesema Rais Magufuli.